Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:01

Marekani 'yasikitishwa' na mswada wa kupinga mapenzi ya jinsia moja Ghana


PICHA YA MAKTABA: Wanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja Ghana.
PICHA YA MAKTABA: Wanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja Ghana.

Marekani Jumatano ilisema "imefadhaishwa mno" na kupitishwa kwa mswada wa sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, na bunge la Ghana, na kuhimiza utathminiwe upya, ili kubaini kama unafuata katiba ya nchi hiyo. 

Bunge la Ghana, Jumatano lilipitisha sheria ambayo ilizidisha ukandamizaji dhidi ya haki za watu wa mapenzi ya jinsia moja, maarufu kama LGBTQ, na wale wanaounga mkono usagaji, ushoga au utambulisho mwingine usio wa kawaida wa kijinsia, katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Mapenzi ya jinsia moja yalikuwa tayari yameharamishwa, na yule ambaye angepatikana na hatia, angeadhibiwa kwa hukumu ya hadi miaka mitatu gerezani.

Mswada huo sasa pia unatoa kifungo cha hadi miaka mitano jela kwa "uungaji mkono kwa makusudi, ufadhili au usaidizi wa shughuli za LGBTQ+."

"Mswada huo unalenga mtu yeyote ambaye anajitambulisha tu kama LGBTQI+, pamoja na rafiki yoyote, familia, au mwanajumuiya ambaye hatawaripoti washukiwa," wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema katika taarifa.

Muungano wa viongozi wa Kikristo, Kiislamu, na kitamaduni nchini Ghana uliunga mkono mswada huo, ambayo iwapo utaidhiniswha na raisa utakuwa mojawapo ya sheria kali zaidi za aina yake barani Afrika.

Kufuatia kura hiyo bungeni, muswada huo utawasilishwa kwa Rais Nana Akufo-Addo ambapo baada ya hapo ana siku saba kuidhinisha au kukataa kuidhinisha, kwa mujibu wa katiba ya Ghana.

Forum

XS
SM
MD
LG