Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 03:29

Ivory Coast ndio washindi wa AFCON 2024


 Ivory Coast washangilia ushindi wa AFCON.
Ivory Coast washangilia ushindi wa AFCON.

Sebastien Haller alifunga bao la ushindi dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika wenyeji Ivory Coast wakinyakua taji la tatu la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Nigeria kwenye mchezo wa fainali Uwanja wa Alassane Ouattara mjini Abidjan Jumapili (Februari 11).

Ni ushindi ambao haungetarajiwa na wengi siku chache zizlizopita hasa kutokana na kwamba timu hiyo ilipata vipigo viwili katika katika awamu ya makundi, kikiwemo kile cha mabao 4-0 kutoka kwa Equatorial Guinea, kabla ya kujizatiti katika raundi ya mchujo.

Bao la kichwa la William Troost-Ekong liliiwezesha Nigeria kuongoza kipindi cha kwanza lakini mchezaji machachari wa Ivory Coast, Franck Kessie alisawazisha.

Wenyeji Ivory Coast walilazimika kutoka nyuma mara kadhaa kwenye dimba hilo na walifanya hivyo tena wakati Haller alipoelekeza krosi ya Simon Adingra wavuni, jambo lililomfurahisha sana kocha wake Emerse Fae, ambaye alianza mchuano huo kama msaidizi wa Mfaransa Jean-Louis Gasset aliyetimuliwa.

Mafanikio ya Ivory Coast yanawafanya kuongeza taji la mwaka huu kwa mengine waliyoyapata mwaka wa 1992 na 2015, wakati ushindi huu pia unawaruhusu kuungana na Nigeria kwa ushindi wa tatu wa Kombe la Mataifa kwa jumla.

Ni Misri, Cameroon na Ghana pekee ambazo zimeshinda taji hilo mara nyingi zaidi.

Ivory Coast imekuwa nchi mwenyeji wa kwanza kushinda AFCON tangu 2006.

Forum

XS
SM
MD
LG