Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:15

Misri yaondolewa kwenye michuano ya Afcon


Mchezaji wa Misri Mohamed Salah, KUSHOTO, kwenye mechi ya awali.
Mchezaji wa Misri Mohamed Salah, KUSHOTO, kwenye mechi ya awali.

Mabingwa mara 7 kwenye michuano ya Afcon Misri, wakiwa hawana nyota wao Mohamed Salah Jumapili wameondolewa kwenye michuano inayoendelea Ivory Coast, baada ya kupoteza kwenye penalty 8-7 dhidi ya DRC.

Muda wa ziada wa mechi yao ulimalizika kwa 1-1 wakati Meschack Elia akipatia DRC goli kwenye dakika ya 37, huku Mostafa Mohamed akisawazisha kwa upande wa Misri.

Salah ambaye ni nyota wa Liverpool alijeruhiwa awali wakati wa mechi dhidi ya Ghana, wakati timu yake ikisema kwamba anahitaji kupumzika, na huenda akerejea uwanjani, iwapo Misri itafika kwenye fainali.

Wachezaji wengine mashuhuri ambao hawakuwa uwanjani kutokana na majeraha pia ni pamoja na Mohamed el Shenawy wa misri , anayesemekana kuwa mlinda lango bora zaidi wa Afrika, pamoja na mchezaji sugu wa DRC Gael Kakuta.

DRC sasa itamenyana na Guinea ambao walishinda Equatorial Guinea 1-0 mapema Jumapili.

Jumatatu mechi zinazosubiriwa kwa hamu ni ile ya Cape Verde dhidi ya Mauritania, lakini zaidi ni ile kati ya bingwa watetezi Senegal na Ivory Coast, baadaye saa 9 jioni kwa saa za huko.

Forum

XS
SM
MD
LG