Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:36

Matumaini ya Ivory Coast yaendelea kuongezeka baada ya kucharaza Senegal Jumatatu


Timu ya Senegal iliyocharazwa na Ivory Coast Jumatatu
Timu ya Senegal iliyocharazwa na Ivory Coast Jumatatu

Jumatatu Ivory Coast imeshangaza bingwa watetezi Senegal, baada kushindwa kwenye penalti na kwa hivyo kuinua matumaini ya kuelekea kwenye fainali wakiwa nyumbani kwao.

Wiki iliopita, Ivory Coast walionekana kutokuwa na matumaini ya kufaulu kwenye muondoano wa makundi, lakini sasa wamefaulu kuingia kwenye robo fainali baada ya kupiga Senegal 5-4. Awali kwenye muda wa kawaida pamoja na wa ziada, walitoka draw ya 1-1.

Sasa basi timu za kutazama kwa karibu hivi Jumanne ni majirani Mali na Burkina Faso, kwenye muondoano wa 16 bora, katika uwanja wa kaskazini wa Ivory Coast wa Korhogo. Baadaye mida ya saa tisa alasiri, Morocco watamenyana na Afrika Kusini, katika uwanja wa Pokou, mjini San Pedro.

Awali Jumatatu Cape Verde walishinda kwenye muondoano wa Afcon kwa mara ya kwanza katika historia baada ya goli la misho mwisho la penalty kutoka kwa Ryan Mendes kuwaweka kwenye 1-0 didhi ya Mauritania mjini Abidjan.

Forum

XS
SM
MD
LG