Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast na kocha wao Emerse Fae walizawadiwa pesa na nyumba za kifahari katika hafla iliyosimamiwa na Rais wa nchi hiyo Jumanne kusherekea ushindi wao katika fainali ya kombe la mataifa barani Afrika.
Sebastien Haller alifunga bao la ushindi dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika wenyeji Ivory Coast wakinyakua taji la tatu la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Nigeria kwenye mchezo wa fainali Uwanja wa Alassane Ouattara mjini Abidjan Jumapili (Februari 11).
Kocha wa Ivory Coast Emerse Fae, alielezea ushindi wa timu yake kwenda hadi fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kuwa "kama ndoto" baada ya wenyeji hao wa michuano ya mwaka 2024 kuwalaza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 1-0 katika mechi ya mchujo Jumatano.
Timu ya Nigeria itakutana na Cameroon Jumamosi katika uwanja wa Felicia wa Abidjan, katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2024. Pambano linalosubiriwa kwa hamu.
Equatorial Guinea iliwashangaza wengi Jumatatu, ilipoweka historia katika Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, kwa kuwalaza wenyeji Ivory Coast, mabao manne kwa nonge na kushinda katika Kundi A, na hivyo kutinga hatua ya 16 bora.
Kocha wa Morocco Walid Regragui alisema Jumapili kwamba alifanya makosa wakati timu yake ilipotoka sare ya 1-1 katika michuano ya Kundi F ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Timu ya taifa ya Tanzania ilipoteza nafasi ya kuandika historia ya kupata ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Afcon dhidi ya Zambia waliokuwa wamebaki na wachezaji 10 katika mechi ya kundi D na kutoka sare ya bao 1-1 katika uwanja wa San Pedro Ivory Coast.
Algeria walipata bao la kusawazisha katika dakika za lala salama na kuepuka kufungwa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Jumamosi na kupata sare ya 2-2 na Burkina Faso katika Kundi D mjini Bouake.
Michuano ya 34 ya kandanda ya bara la Afrika inaendelea nchini Ivory Coast. Msururu wa vipaji vya kandanda barani humo vitaonyeshwa katika michuano hii ambayo inadumu kuanzia Januari 13 hadi Februari 11. Baadhi ya wachezaji watakaotazamwa katika michuano hii ni kama ifuatavyo.
Wakati tukiendelea kuangazia michuo ya Afcon inayoendelea nchini Ivory Coast ni kwamba Misri Alhamisi imejitahidi kweli kweli kupata draw ya 2-2 dhidi ya Ghana licha ya kupoteza nyota wake Mohamed Salah katika nusu ya kwanza kutokana na jeraha.
Kwenye michuoano ya Afcon inayeondelea Ivory Coast ni kwamba moja ya mechi za kutarajia Alhamisi ni kati ya Equatorial Guinea na Guinea Bissau kwenye uwanja wa Alassane Ouattara saa nane saa za huko kwenye kundi A.
Mchezaji matata wa Senegal Lamine Camara ameheshimisha Senegal Jumatatu wakati timu hiyo ikijitahidi kutetea ubingwa wake kwenye michuoano ya Afcon inayoendelea Ivory Coast.
Pandisha zaidi