Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 14:21

Kocha wa Morocco akiri kufanya makosa baada ya timu yake kutoka sare 1-1 na DRC


Kocha wa Morocco Walid Regragui
Kocha wa Morocco Walid Regragui

Kocha wa Morocco Walid Regragui alisema  Jumapili kwamba alifanya makosa wakati timu yake ilipotoka sare ya 1-1 katika michuano ya Kundi F ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Katika mechi hiyo Achraf Hakimi alihakikisha kwamba timu ya Atlas Lions wameanza vyema wakati katika dakika ya sita, alipoupachika mpira wavuni katika mji wa pwani ya kusini magharibi wa San-Pedro, nchini Ivory Coast.

Lakini kwa upande wa DRC, hata baada ya Cedric Bakambu, kukosa penalti ya timu yake ya Leopards, walisawazisha dakika ya 76 kupitia mkwaju wa Silas Katompa Mvumpa.

Zambia, ikiwa na wachezaji kumi baadaye ilitoka sare ya bao moja kwa moja na Tanzania na kuziacha timu zote nne zikiwa na nafasi ya kutinga hatua ya mtoano.

Hali ilikuwa hiyo hiyo katika Kundi E, baada ya Afrika Kusini kuichazaza Namibia mabao manne kwa sufuri katika mji wa Korhogo, ambapo mkongwe Themba Zwane alifunga mara mbili.

Morocco, ambao miaka miwili iliyopita wakiwa Qatar walikuwa wa kwanza kuingia nusu fainali Kombe la Dunia kutoka Afrika, wana pointi nne katika mechi mbili, DR Congo na Zambia mbili kila moja na Tanzania moja.

Regragui, aliyetangazwa kuwa Kocha Bora wa Afrika wa Mwaka katika tuzo za kila mwaka za CAF mwezi uliopita kutokana na mafanikio yake katika Kombe la Dunia, aliwaambia waandishi wa habari kwamba mabadiliko aliyoyafanya katika kipindi cha pili hayakufaulu.

Jumatatu, Guinea Bissau watamenyana na Nigeria, huku Equitorial Guinea wakapambana na Ivory Coast. Baadaye, Msumbiji watatoana jasho na Ghana huku Cape Verde wakishindana na Misri.

Forum

XS
SM
MD
LG