Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:45

Misri yatoka sare na Ghana licha ya kupoteza Salah kutokana na jeraha


Mchezaji wa Ghana Mohammed Kudus akisherehekea baada ya kupata goli lake la pili kwenye michuano ya Afcon
Mchezaji wa Ghana Mohammed Kudus akisherehekea baada ya kupata goli lake la pili kwenye michuano ya Afcon

Wakati tukiendelea kuangazia michuo ya Afcon inayoendelea nchini Ivory Coast ni kwamba Misri Alhamisi imejitahidi kweli kweli kupata draw ya 2-2 dhidi ya Ghana licha ya kupoteza nyota wake Mohamed Salah katika nusu ya kwanza kutokana na jeraha.

Kwa upande wa Ghana, magoli yote mawili yalipachikwa wavuni na Mohammed Kudus, dakika 20 baada ya Salah kuondoka uwanjani, kwenye mechi hiyo ya kundi B katika uwanja wa Felix Houphouet Boigny. Misri sasa inaongoza kwa pointi moja tu baada ya kutoka sare mfululizo, wasi wasi mkubwa ukiwa kwenye afya ya tegemeo lake kuu, Mohamed Salah.

Kocha wao Rui Victoria amesema kuwa haijabainishwa vikamilifu jeraha lake ni lipi, lakini wanatumai kwamba ataweza kurudi uwanjani kwa haraka. Basi hivi leo mechi za kutazamia kwa karibu ni zile za Senegal dhidi ya Cameroon, saa 6 za mchana na Guinea dhidi ya Gambia baadaye saa tisa. Najua kwamba kwa uhakika unasubiri kwa hamu kuona mambo yatavyokuwa kati ya Tanzania na Zambia, ifikapo Jumapili.

Forum

XS
SM
MD
LG