Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 19:14

Nigeria kumenyana na Ivory Coast Alhamisi baada ya Tanzania kucharazwa 3-0 na Morocco Jumatano


AFCON
AFCON

Kwenye michuoano ya Afcon inayeondelea Ivory Coast ni kwamba moja ya mechi za kutarajia Alhamisi ni kati ya Equatorial Guinea na Guinea Bissau kwenye uwanja wa Alassane Ouattara saa  nane saa za huko kwenye kundi A.

Wakati huo huo, wenyeji Ivory Coast watatoana vumbi na Nigeria kwenye uwanja huo huo baadaye saa 11 jioni.

Kwenye kundi la B, Misri watamenyana na Ghana saa mbili za usiku kwenye uwanja wa michezo wa Felix Houphouet Boigny mjini Abidjan.

Jumatano mechi mbili muhimu zilifanyika ambapo ile ya ufunguzi ya kundi F iliishia kwa Tanzania kucharazwa magoli matatu kwa nonge na Morocco.

Cameroon ni moja ya timu zinazotazamwa kwa karibu ikionekana kuwa tishio kubwa kwa mabingwa watetezi Senegal.

Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pia kutoka kundi F walitoka sare ya 1-1.

Sasa mechi ya kusubiri kwa hamu Alhamisi ni ile ya Nigeria dhidi ya Ivory Coast.

Forum

XS
SM
MD
LG