Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 09, 2024 Local time: 23:18

Cape Verde yaishangaza Ghana mshindi mara nne wa zamani


AFCON 2023: Cape Verde yaishangaza Ghana
please wait

No media source currently available

0:00 0:00:11 0:00

AFCON 2023: Cape Verde yaishangaza Ghana

Kocha wa Cape Verde Pedro 'Bubista' Brito amepongeza ladha maalum ya timu yake baada ya ushindi wao wa kushtukiza wa bao 2-1 dhidi ya mabingwa mara nne wa zamani Ghana katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika  mjini Abidjan.

Kocha wa Ghana

Tunataka kuonyesha ulimwengu kwamba tunaweza kushindana katika soka na timu zote barani Afrika. Naye kocha wa Ghana Chris Hughton anaomboleza usiku wa kukatisha tamaa na kusema kuwa hatuna namna ila kuhakikisha kuwa tunapata matokeo mazuri katika mchezo wetu ujao dhidi ya Misri.

Michuano ya 34 ya mashindano makubwa kabisa barani Afrika imeanza nchini Ivory Coast kuanzia Januari 13 hadi Februari 11 2024 katika maeneo ya Yamoussoukro, Bouake, San Pedro, na Korhogo.

Mchezo wa ufunguzi ulikuwa kati ya wenyeji Ivory Coast na Guinea-Bissau siku ya Jumamosi tarehe 13 Januari 2024 kwenye Uwanja wa Olimpiki wa Alassane Ouattara wa Ebimpe, mjini Abidjan.

Katika historia ya mashindano hayo, ndugu sita wamefanikiwa kutwaa kombe hilo mpaka sasa: nao ni Italo na Luciano Vassalo mwaka 1962, Albert Bwanga na Robert Kazadi wa DRC mwaka 1974, André na François Biyik wa Cameroon mwaka 1988 na Christopher na Felix Katongo wa Zambia mwaka 2012, na kwa Ivory Coast ni Yaya na Kolo Toure mwaka 2015.

Hossam na Ibrahim Hassan wa Misri walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1986 na 1998 kwa pamoja.

Mwaka 2024 itakuwa Kombe la sita la Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies CAF ambalo ndugu watoto wa Abedi Pele watacheza pamoja. Mwaka 2015, André na Jordan Ayew walikuwa wakikaribia kushinda taji lao la kwanza lakini hawakuweza kuwaangusha miamba Ivory Coast wakati wa mikwaju ya penalti isiyoisha.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari na AP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG