Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 19:00

Senegal yaanza kwa kuonyesha ubabe wake kwenye michuano ya Afcon


Wachezaji wa timu ya Senegal wakisherehekea ushindi wao dhidi ya Gambia, Jumatatu.
Wachezaji wa timu ya Senegal wakisherehekea ushindi wao dhidi ya Gambia, Jumatatu.

Mchezaji matata wa Senegal Lamine Camara ameheshimisha Senegal Jumatatu  wakati timu hiyo ikijitahidi kutetea ubingwa wake kwenye michuoano ya Afcon inayoendelea Ivory Coast.

Hata hivyo mambo yaliwaendea mrama Algeria na Cameroon wakati wa mechi zao za ufunguzi.

Timu ya Senegal yake Dadio Mane ina matumaini ya kuhifadhi ubingwa wake ilioupata Cameroon miaka miwili iliyoita, wakati ikonekana kuwa na nguvu nyingi dhidi ya jirani zake Gambia ambao walichaza kwenye nusu ya pili wakia na wachezaji 10 pekee.

Huenda sasa kibarua kikawa kigumu kwa Senegal kwenye mechi yao inayofuata kwenye kundi C, pale watakapomenyana na Cameroon ambao ni washindi mara 5 wa michuano hiyo.

Algeria ambao walikuwa washindi wa Afcon 2019 pia wamejiunga kwenye orodha ya vigogo waliofanya vibaya kwenye mechi za ufunguzi, wakifuata nyayo za Cameroon, Nigeria, Misri na Ghana baada ya kutoka draw ya 1-1 dhidi ya Angola mjini Bouake.

Mechi ya kutazama kwa karibu ni ile kati ya Burkina Faso na Mauritainia Jumanne.

Forum

XS
SM
MD
LG