Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 20, 2024 Local time: 20:39

Blinken kufanya ziara katika nchi nne za Afrika


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alipowasili Cairo, Misri Mai 26, 2021. Picha na Alex Brandon/Pool via REUTERS
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alipowasili Cairo, Misri Mai 26, 2021. Picha na Alex Brandon/Pool via REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken wiki ijayo atayatembelea mataifa manne ya Cape Verde, Ivory Coast, Nigeria, na Angola wiki ijayo, wizara hiyo imesema katika taarifa yake. Hii ni ziara yake ya nne katika bara hilo.

Ziara hiyo inakuja baada ya ile ya mwaka jana ya maafisa 17 wa ngazi ya mawaziri, ikiwa ni kufuatilia mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika uliofanyika Washington 2022.

Rais Joe Biden pia ameelezea azma yake ya kulitembelea bara la Afrika mwaka huu, lakini hakuna mipango kamili iliyotangazwa.

Wakati alipokuwa makamu wa rais Joe Biden na mkewe Jill Biden waliweka shada la maua katika eneo lilipokuwa ubalozi wa Marekani huko Nairobi
Wakati alipokuwa makamu wa rais Joe Biden na mkewe Jill Biden waliweka shada la maua katika eneo lilipokuwa ubalozi wa Marekani huko Nairobi

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje, Matthew Miller amesema ziara ya siku sita Blinken itaangazia jinsi Marekani ilivyoongeza ushirikiano kati ya Marekani na Afrika tangu mkutano huo ufanyike, yakiwemo maeneo kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, chakula, na usalama wa afya.

“Pia atasisitiza ushirikiano wa baadaye wa kiuchumi na jinsi Marekani inavyowekeza katika miundo mbinu barani Afrika ili kuboresha biashara kati ya Marekani na Afrika, kufungua nafasi za ajira nchini Marekani na Afrika, na kuisaidia Afrika katika ushindani kwenye soko la dunia” amesema Miller.

Alipoulizwa kama kukabiliana na ushawishi wa China itakuwa mada kuu, waziri mdogo wa mambo ya nje wa kwa masuala ya Afrika, Molly Phee alisema hii ni zaidi ya mkazo unaotolewa na vyombo vya habari.

Rais Biden akishiriki chakula cha jioni na viongozi waliohudhuria mkutano wa ushirikiano baina ya Marekani na Afrika uliofanyika Washington Desemba 14,2022.
Rais Biden akishiriki chakula cha jioni na viongozi waliohudhuria mkutano wa ushirikiano baina ya Marekani na Afrika uliofanyika Washington Desemba 14,2022.

Kama China haikuwepo, tungekuwa tukishiriki kikamilifu Afrika,”amesema. “Afrika ni muhimu kwa ajili yake yenyewe, na ni muhimu kwa manufaa ya Wamarekani”

Phee ameitaja miradi mikubwa ya miundo mbinu ambayo inashirikiana na Angola na Cape Verde. Amesema habari nyingi mbaya zinakuja kutoka Afrika, na ziara ya Blinken itaangazia mazuri.

“Nafikiri naweza kuangazia uwezo mkubwa wa waafrika, hususani vijana. Inaweza kuonyesha aina ya ushirikiano tunaotazamia, kwa mfano, ushirikiano wetu na Angola katika anga ya juu.”

Phee amesema wakati mashindano ya kandanda ya mataifa ya Afrika (AFCON) yakiendelea, Blinken ana matumaini ya kuhudhuria mechi wakati akiwa nchini Ivory Coast.

Forum

XS
SM
MD
LG