Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 20, 2024 Local time: 21:02

Netanyahu atofautiana na Marekani kuhusu kubuniwa kwa taifa la Palestina


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu .
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu .

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu  Alhamisi amesema kwamba ameambia Marekani kuwa anapinga msimamo wa muda mrefu wa Washington, wa kuundwa kwa taifa la Palestina, kama  sehemu ya makubaliano ya baada ya kumalizika kwa vita vya Israel, dhidi ya wanamgambo wa Hamas.

Maafisa kutoka kwenye serikali ya mrengo wa kulia ya Israel pia wameeleza upinzani wao wa kuundwa kwa taifa huru la Palestina linalopakana na Israel. Hata hivyo hotuba ya Netanyahu kupitia kikao na wanahabari kilichorushua na vyombo vya habari kote nchini, inaonekana kufichua wazi wazi tofauti iliyopo na Marekani, ambaye ni mshirika mkubwa zaidi wa Israel kwenye mapigano hayo.

Msemaji wa Baraza la Kitaifa la Usalama wa Marekani John Kirby hata hivyo amepuuzia matamshi ya Netanyahu. “Hili si tangazo jipya kutoka kwa Waziri Mkuu Netanyahu. Hata hivyo tunaliangia kwa mtazamo tofauti,” amesema Kirby.

Forum

XS
SM
MD
LG