Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 03:01

Mazungumzo ya Qatar huenda yakatatua mzozo wa Gaza, Marekani yasema


Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Marekani, John Kirby.
Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Marekani, John Kirby.

Marekani imesema Jumanne kwamba ina matumaini kwamba mazungumzo yanayo ongozwa na Qatar yatafikia mkataba mpya kuelekea kuachiliwa kwa mateka walioshikiliwa na Hamas kwenye Ukanda wa Gaza, kwa mabadilishano ya sitisho la mapigano kati ya Hamas na Israel.

“Sitaki kusema mengi hadharani tunapoendelea na mazungumzo hayo, lakini tuna imani kwamba yatazalisha matunda karibuni,” amesema John Kirby, msemaji wa baraza la kitaifa la Usalama hapa Marekani, wakati alipokuwa akizungumza na wanahabari kwenye Ikulu ya Marekani.

Zaidi ya mateka 100 waliachiliwa wakati wa sitisho la muda la mapigano la Novemba, lakini takriban 132 wanaaminika kuendelea kushikiliwa na Hamas ndani ya Gaza, yakiwemo mabaki ya takriban darzeni 2 waliofia huko.

Wakati huo huo vita hivyo vikiwa vimepita siku 100 wiki hii, vifaru vya Israel vimeanza kushambulia tena maeneo ya kaskazini mwa Gaza Jumanne, baada ya kusitisha kwa muda tangu wiki iliopita. Milipuko mikubwa ilionekana kwenye anga ya kaskazini mwa Gaza kutoka kwenye mpaka wa Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG