Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:50

AFCON: Wenyeji Ivory Coast katika hatari ya kuondoka baada ya kutingwa 4-0 na Equitorial Guinea


Ivory Coast AFCON Soccer
Ivory Coast AFCON Soccer

Equatorial Guinea iliwashangaza wengi Jumatatu, ilipoweka  historia katika  Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON,  kwa kuwalaza wenyeji Ivory Coast, mabao manne kwa nonge na kushinda katika Kundi A, na hivyo kutinga hatua ya 16 bora.

Walijumuishwa katika awamu ya muondoano na Nigeria, vinara wa Kundi Ba, huku washindi wengine, Cape Verde, wakiungana na mabingwa mara saba wa kinyang’anyiro hicho, Misri, kwenye michuano itakayofuata.

Nigeria waliwashinda Guinea-Bissau 1-0, na kumaliza wakiwa wa pili nyuma ya Equitorial Guinea, huku sare ya 2-2 kati ya Cape Verde na Misri, ikiruhusu timu hizo kusonga mbele.

Ghana ilipigwa mabao mawili katika muda wa ziada na kutoka sare ya 2-2 na Msumbiji, na, ikiwa na pointi mbili pekee, huenda isiwe miongoni mwa timu nne bora zilizo katika nafasi ya tatu ambazo pia zitafuzu.

Leo Jumanne, Gambia watapambana na Cameroon, huku Guinea Conakry wakimenyana na Senegal, wakati Mauritania nao wakionyeshana kivumbi na Algeria, ambapo baadaye, Angola na Burkina faso wataingia uwanjani kutoana jasho.

Forum

XS
SM
MD
LG