Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:05

Wachezaji wa timu ya soka ya Ivory Coast wazawadiwa pesa na nyumba za kifahari


Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast wakifurahia ushindi katika fainali ya kombe la AFCON
Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast wakifurahia ushindi katika fainali ya kombe la AFCON

Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast na kocha wao Emerse Fae walizawadiwa pesa na nyumba za kifahari katika hafla iliyosimamiwa na Rais wa nchi hiyo Jumanne kusherekea ushindi wao katika fainali ya kombe la mataifa barani Afrika.

Tembo wa Ivory Coast waliishinda Nigeria katika fainali siku ya Jumapili na kunyakua taji hilo kwa mara ya tatu.

Kila mchezaji alipewa milioni 50 za sarafu ya CFA na nyumba ya kifafari yenye thamani sawa na pesa hizo.

Kocha Fae alipewa milioni 100 za sarafu ya CFA kwa kuongoza vizuri wachezaji wake baada ya kuchukua nafasi ya kocha mkuu aliyetimliwa Jean Louis Gasset katikati ya mashindano kufuatia kipigo kibaya cha mabao 4-0 dhidi ya Equatorial Guinea.

“Mmeleta furaha kwa wanainchi wote wa Ivory Coast, hongera, hongera,” alisema Rais Alassane Ouattara.

Forum

XS
SM
MD
LG