Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 20:56

Watu wawili waangamia kwenye ajali ya ndege ya Nairobi


Picha ya maktaba ya mabaki ya ndege ilioanguka.
Picha ya maktaba ya mabaki ya ndege ilioanguka.

Polisi nchini Kenya wamesema Jumanne, kwamba watu wawili wamekufa kwenye ajali kati ya ndege ya chuo cha urubani, na ile ya abiria, kwenye mji mkuu wa Nairobi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, tukio hilo lilitokea mwendo wa saa nne asubuhi saa za huko, pale ndege ya chuo cha urubani ilipogongana na ile ya abiria ya kampuni ya Safarilink, idara ya mamlaka ya anga ya Kenya imesema katika taarifa.

Safarilink imesema kwamba hakuna abiria aliyejeruhiwa kwenye ndege yao, iliyokuwa ikielekea kwenye mji wa kitalii wa Diani, uliopo pwani ya Kenya. Kamanda wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei hata hivyo amethibitisha kuwa mwanafunzi wa urubani pamoja na mwalimu wake wameangamia kwenye ajali hiyo , bila kutoa taarifa zaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG