Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:27

Wanajeshi wa Ufaransa kwendelea kuwepo Chad - Macron


Wanajeshi wa Chad.
Wanajeshi wa Chad.

Ufaransa itabakisha wanajeshi wake nchini Chad, iliyo chini ya utawala wa kijeshi, huku ikiwaondoa kwingineko barani Afrika, kutokana na mvutano na tawala za kijeshi, mjumbe wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Alhamisi. 

Ushawishi wa Ufaransa katika makoloni yake ya zamani Afrika Magharibi umepungua huku watawala wa kijeshi waliokuwa wakipambana na uasi wa wanajihadi nchini Mali, Burkina Faso na Niger wakiwafukuza wanajeshi wa Ufaransa na kuimarisha uhusiano na Russia.

Takriban wanajeshi 1,000 wa Ufaransa wanapiga kambi nchini Chad, ikiwa idadi ndogo ya wanajeshi katika nchi mshirika inayoongozwa na Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno tangu mwaka wa 2021.

“Bila shaka tutabaki” nchini Chad, alisema Marie Bockel, mjumbe wa Macron barani Afrika ambaye alipewa jukumu la kujadili sera mpya ya kijeshi ya Ufaransa barani Afrika.

Macron aliomba mazungumzo na viongozi wa Chad juu ya “mabadiliko” ya kupelekwa kwa wanajeshi wa Ufaransa “kukabiliana vyema na changamoto za kiusalama na za kijeshi katika kanda hiyo, Bockel aliongeza baada ya kukutana na Deby Itno mjini N’Djamena.

Bockel alisema pia alimuelezea Deby Itno kuwa Ufaransa inaipongeza Chad kwa kurejea kwenye utawala wa kiraia, mchakato ambao ulianza baada ya kiongozi huyo wa kijeshi kuchukua madaraka kufuatia zaidi ya miongo mitatu ya utawala wa kimabavu wa baba yake.

Deby Itno atagombea kwenye uchaguzi wa rais wa tarehe 6 Mei na kurejesha utawala wa kiraia, na ana matumaini ya kushinda, huku viongozi wakuu wa upinzani wakilazimishwa kwenda uhamishoni au kuuawa.

Forum

XS
SM
MD
LG