Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 21:24

Maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya Paris yakamilika kwa wakati, kijiji chazinduliwa


Rais wa Kamati ya Maandalizi ya Paris ya Olimpiki 2024 Tony Estanguet, Rais wa Ufaransa Macron, Waziri wa Michezo na Olimpiki Amelie Oudea-Castera wakihudhuria ufunguzi wa Kijiji cha Olimpiki huko Saint-Denis, Feb. 29, 2024.
Rais wa Kamati ya Maandalizi ya Paris ya Olimpiki 2024 Tony Estanguet, Rais wa Ufaransa Macron, Waziri wa Michezo na Olimpiki Amelie Oudea-Castera wakihudhuria ufunguzi wa Kijiji cha Olimpiki huko Saint-Denis, Feb. 29, 2024.

Waandaaji wa michezo ya Olimpiki ya Paris waliingia katika kijiji kipya cha wanariadha kilichoandaliwa Alhamisi katika muda ulipangwa, ikiimarisha uthabiti unaokua kwamba wataweza kuwa tayari kwa michezo hiyo kufanyika.

Katika sherehe za uzinduzi wa kijiji hicho huko kaskazini ya Paris, muandaaji mkuu Tony Estanguet alipokea ufunguo wa ishara ya ufunguzi huo kwa ajili ya uwanja huo mbele ya viongozi kadhaa akiwemo Rais Emmanuel Macron.

“Ni ishara ya kuwa tumetekeleza ahadi zetu,” Macron aliwaambia waandishi wa habari, ambaye aliwaambia wafanyakazi wanatakiwa kuwa na “fahari” ya kukabidhi kijiji hicho “kwa wakati na katika kiwango cha bajeti iliyowekwa.”

Waandaaji watatumia miezi minne ijayo kukamilisha mahitaji ya kijiji hicho kwa kuweka zaidi ya vifaa 300,000 vya samani na kupamba kabla ya kuwasili wanariadha wa kwanza kuanzia Julai 18.

Eneo hilo lina takriban majengo ya ghorofa fupi 40 na itajumuisha mgahawa utakao kuwa wazi saa 24, baa isiyokuwa na pombe na sehemu ya starehe, pamoja na vyumba vya mazoezi.

Serikali ya Ufaransa imechangia euro milioni 646 (dola milioni 700) katika fedha za umma, huku kiwango kilichobakia kikitolewa na makampuni makubwa ya biashara ya majumba ambazo zimejenga maeneo mbalimbali katika eneo hilo la hekta 52.

Forum

XS
SM
MD
LG