Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:01

Afrika Kusini: Nyota wa zamani wa Olimpiki wa walemavu aachiliwa kwa msamaha


FILE PHOTO: Pictures of the Decade
FILE PHOTO: Pictures of the Decade

Nyota wa zamani wa Olimpiki wa Walemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, aliyefungwa mwaka 2014 kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp, ataachiliwa kwa msamaha kuanzia Januari 5, 2024.

Hayati Reeva Steenkamp
Hayati Reeva Steenkamp

Awali alifungwa jela miaka mitano mwaka 2014 kwa kuua bila kukusudia na mahakama kuu lakini Mahakama ya Juu ya Rufaa mwishoni mwa 2015 ilimkuta na hatia ya mauaji baada ya rufaa ya waendesha mashtaka.

Pistorius - anayejulikana kama "Blade Runner" kwa miguu yake bandia , alimpiga risasi mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 29 na mhitimu wa sheria kupitia mlango wa bafuni katika Siku ya Wapendanao mwaka 2013, na baadaye aliiambia mahakama mara kwa mara kwamba alimdhania kuwa mvamizi. .

Idara ya Huduma za Urekebishaji ilitangaza msamaha huo mnamo Novemba, na kuongeza kuwa Pistorius atamaliza kifungo chake kilichosalia katika mfumo wa marekebisho ya jamii na atafuatiliwa.

Sababu kadhaa kwa kawaida huzingatiwa na bodi ya msamaha, ikiwa ni pamoja na asili ya uhalifu, uwezekano wa kufanya tena makosa, mwenendo gerezani, ustawi wa kimwili na kiakili na vitisho vinavyoweza kumkabili mfungwa akiachiliwa.

Pistorius alinyimwa msamaha mapema mwaka jana, baada ya kuamuliwa kuwa hajamaliza muda wa chini wa kukaa gerezani ambao unatakiwa kuzingatiwa kwa msamaha.

Hata hivyo, Mahakama ya Katiba ilisema mwezi Oktoba kuwa Pistorius alikuwa ametumikia nusu ya kifungo chake kufikia Machi 21, jambo ambalo lilimaanisha kuwa anastahili, baada ya hukumu yake kurejeshwa hadi Julai 2016 badala ya Novemba 2017.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG