Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:53

Jaji wa Afrika Kusini atupilia mbali la ombi la rufaa la Oscar Pistorius


Oscar Pistorius akitoka mahakamani June 14, 2016.
Oscar Pistorius akitoka mahakamani June 14, 2016.

Jaji mmoja wa Afrika Kusini ametupilia mbali ombi kutoka kwa waendesha mashitaka kupinga hukumu ya kwenda jela miaka sita ya Oscar Pistorius kwa kumuuwa mchumba wake.

Jaji Tokozile Masipa alisema Ijumaa alifikiri kwamba ombi hilo la kukata rufaa lilikuwa na nafasi ndogo sana ya mafanikio.

Pistorius alihukumiwa kwa kumuuwa mchumba wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake Pretoria February 2013.

Hukumu hiyo ya miaka 6 ilikuwa ni ndogo sana kuliko ile ya mitaa 15 iliyoombwa na waendesha mashitaka.

Mwendesha mashitaka Gerie Nel alisema kwamba hukumu hiyo ilikuwa ni ya kustusha kwamba amepewa ahueni kubwa na kwamba jamhuri ingepewa nafasi ya kuomba hukumu ndefu zaidi. Wakili wa utetezi Barry Roux amesema kwamba hatua za kisheria zimeangaliwa zote mpaka mwisho.

Wakati wa kesi Pistorius amesema kwamba alipiga risasi kwenye mlango wa bafuni akihisi kwamba ameingiliwa Waendesha mashitaka walisema kwamba mwanamichezo huyo alimuuwa mchumba wake kwa makusudi baada ya mabishano makali.

XS
SM
MD
LG