Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:10

Oscar Pistorius arudishwa gerezani


Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akiondoka katika mahakama kuu ya Pretoria, tarehe 14, Juni mwaka 2016. Picha na MARCO LONGARI / AFP.
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akiondoka katika mahakama kuu ya Pretoria, tarehe 14, Juni mwaka 2016. Picha na MARCO LONGARI / AFP.

Bingwa wa Olimpiki ya Walemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius hakupewa msahama siku ya Ijumaa baada ya kuomba kuachiliwa mapema kutoka gerezani, muongo mmoja baada ya kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp, mawakili na mamlaka wamesema.

Idara ya Huduma za Magereza imesema bodi ya msamaha iligundua kuwa Pistorius hajakamilisha kiwango cha chini cha kifungo chake kinachohitajika ili kutolewa mapema.

"Tulishauriwa kwa wakati huu kwamba ombi lako limekataliwa" hili litaangaliwa tena katika kipindi cha mwaka mmoja, wakili wa familia ya muathirika Tania Koen, aliliambia shirika la habari la AFP.

Hatuo hiyo imekuja kama mshangao na imeelezewa na wataalamu wa kisheria kuwa “haukuwa wa kawaida", hapo awali idara ya huduma ya magereza ilisema Pistorius alistahili kuachiliwa mapema kwa kuwa ameshatumikia zaidi ya nusu ya kifungo chake.

Pistorius alimuua mpenzi wake mwanamitindo Reeva Steenkamp, kwa kumpiga risasi nne kupitia mlango wa bafuni alfajiri ya siku ya wapendanao mwaka 2013. Tukio ambalo lilitokea kwenye nyumba yake yenye ulinzi mkali iliyoko katika mji wa Pretoria , mauaji ambayo yaliushangaza ulimwengu.

Kikao cha kusikiliza ombi lake la msamaha siku ya Ijumaa asubuhi katika jela iliyo nje kidogo ya mji mkuu ambako Pistorius mwenye umri wa miaka 36 anatumikia kifungo chake.

Wazazi wa Steenkamp, ambao wamekuwa wakipinga kuachiliwa mapema kwa mwanariadha huyo wa zamani, wamesema hawaamini kwamba alisema ukweli kuhusu kile kilichotokea na hajaonyesha majuto, wamefurahishwa na uamuzi.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG