Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:59

Mamia wajitokeza kusindikiza jeneza la bingwa wa riadha Kelvin Kiptum


Sehemu ya watu waliojitokeza kusindikiza jeneza la Alvin Kiptum mjini Eldoret. February 22, 2024.
Sehemu ya watu waliojitokeza kusindikiza jeneza la Alvin Kiptum mjini Eldoret. February 22, 2024.

Mamia ya waombolezaji nchini Kenya, Alhamisi wamesindikiza jeneza la mwanariadha bingwa wa dunia wa mbio ndefu  Kelvin Kitum, wakati lilipokuwa likipekekwa kwenye kijiji chake ambako atazikwa.

Huku wakiimba nyimbo za dini na kushikana mikono, waombolezaji hao waliufuata msafara wa magari uliobeba jeneza hilo kutoka kwenye chumba cha kuhifadhi maiti mjini Eldoret, ukielekea kwenye kijiji chake cha Chepsamo.

Kiptum mwenye umri wa miaka 24 alikufa katika ajali ya barabarani akiwa na kocha wake Gervais Hakizimana mapema mwezi huu, baada ya gari lake kupoteza mwelekeo na kugonga mti. Kiptum alikuwa ameshiriki marathon mara tatu, zote zikiwa miongoni mwa 7 zenye kasi kubwa zilizowahi kurekodiwa katika historia.

Oktoba mwaka jana, Kiptum aliweka rekodi kwenye mbio za marathon za Chicago baada ya kukimbia kwa muda wa saa 2 na sekunde 35, na kwa hivyo kupita saa 2 na dakika 1.09 alizokimbia Eliud Kipchoge.

Kiptum alikuwa na matumaini ya kuvunja ya rekodi ya kukimbia chini ya muda wa saa 2 kwenye mbio za ndefu za Rotterdam hapo Aprili, ambapo pia alitarajiwa kwa mara ya kwanza, angeshiriki katika Olimpiki baadaye mwaka huu mjini Paris. Kama angeshiriki angejikuta akishindana na bingwa mwenzake Eliud Kipchoge.

Forum

XS
SM
MD
LG