Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 21, 2024 Local time: 09:23

Mtoto wa jenerali wa Sudan apata ajali Uturuki


Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ( wa pili kushoto) akipeana mikono na maafisa kabla ya kwenda Uturuki Septemba 13, 2023. Picha na baraza la serikali ya mpito ya Sudan / AFP
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ( wa pili kushoto) akipeana mikono na maafisa kabla ya kwenda Uturuki Septemba 13, 2023. Picha na baraza la serikali ya mpito ya Sudan / AFP

Mtoto wa kiume wa mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan amejeruhiwa vibaya katika ajali ya barabarani nchini Uturuki, ripoti ya chombo cha habari nchini humo imesema.

Mohammed Fattah al-Burhan Rahmane alikuwa akiendesha pikipiki katika mji kuu wa Ankara, wakati alipogongana na gari kubwa siku ya Alhamisi na pikipiki yake kurushwa mita kadhaa, limeripoti shirika la habari la DHA.

Mtoto huyo wa jenerali wa Sudan alihamishwa hospitali ambako amelazwa katika chumba cha watu mahututi, ripoti hiyo iliongeza.

Ubalozi wa Sudani mjini Ankara hhaukujibu mara moja ulipoombwa kutoa maoni.

Tangu mwezi Aprili, Burhan amekuwa vitani na aliyekuwa naibu wake Mohamed Hamdan Daglo, ambaye anaongoza Kikosi cha Msaada wa Dharura (RSF).

Majenerali hao wawili walitofautiana baada ya mapinduzi ya kijeshi ya pamoja ya mwaka 2021 ambayo yalivuruga kipindi tete cha mpito wa kidemokrasia nchini Sudan.

Vita hivyo vimeua maelfu ya watu, ikiwa pamoja na 15,000 katika mji mmoja wa West Darfur, kulingana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Pia umedhoofisha a uchumi, kuharibu miundo mbinu na kuwalazimisha zaidi ya watu milioni nane kukimbia makazi yao, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa

Forum

XS
SM
MD
LG