Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 15:41

Afisa wa juu wa Marekani azionya mamlaka kusitisha usambazaji wa Silaha Sudan


 Linda Thomas-Greenfield akizungumza wakati wa mkutano wa baraza kuu la usalama huko New York Februari 23, 2024. Picha na Charly TRIBALLEAU / AFP
Linda Thomas-Greenfield akizungumza wakati wa mkutano wa baraza kuu la usalama huko New York Februari 23, 2024. Picha na Charly TRIBALLEAU / AFP

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield amezitaka nchi kusitisha usambazaji wa silaha kwa majenerali waliohasimiana wanaopigana vita vya wenyewe kwa wenyewe, amesema wanachochea “vifo, na uharibifu.”

“Mgogoro ambao, wakati ripoti hii inaeleza, inachochewa na silaha zinazosafirishwa kutoka mamlaka chache za kikanda zenye nguvu ambazo lazima ziache” Balozi huyo wa Marekani Umoja wa Mataifa aliwaambia waandishi wa habari Jumatano

Alikuwa akizungumzia ripoti ya mwisho ya jopo la wajumbe watano wataalamu wa masuala ya Sudan, ambao wamelitaka balaza la Usalama kuripoti kuhusiana na uwekaji wa vikwazo wa baraza hilo. Ripoti hiyo imechapishwa wiki hii.

Thomas-Greenfield alielezea matokeo ya ripoti hiyo kama “kuvuruga tumbo” na kusema ripoti hiyo imeelezea ukatili baada ya ukatili."

Ripoti hiyo ya kurasa 52, ilikamilika katikati ya mwezi Januari, imesema vikosi vyote vya jeshi la Sudani (SAF) na waasi wa kikosi cha Msaada wa dharura wana njia za kifedha zinazofadhili vita vyao, akibainisha wanadhibiti biashara karibu yote ya dhahabu nchini Sudan.

Vita vilizuka mwezi April mwaka jana kati ya mkuu wa jeshi la Sudan, jenerali Abdel Fattah Burhan, na kamanda kikosi cha Msaada wa Dharura Mohamed Hamdan Dagalo. Majenerali hao walikuwa washirika katika serikali ya mpito baada ya mapinduzi ya mwaka 2021 lakini walihasimiana kwa ajili ya madaraka.

Forum

XS
SM
MD
LG