Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:27

Viongozi wa Afrika wakutana Addis Ababa


Viongozi wa Afrika wamefungua mkutano wa siku mbili, Jumamosi huku bara hilo likipambana na mapinduzi, mizozo, migogoro ya kisiasa na mivutano ya kikanda.

Kabla ya mkutano huo katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, mkuu wa tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, alitoa tahadhari kutokana na ghasia zinazoyakumba mataifa mengi, barani Afrika na sehemu nyingine za dunia.

Sudan imekuwa katika hali mbaya, Faki amesema, huku pia akiangazia tishio la wenye masimamo mkali nchini Somalia, mivutano ya muda mrefu huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hatari ya ugaidi katika Sahel, na ukosefu wa utulivu wa mara kwa mara nchini Libya.

Mkutano huo mfupi uliolenga kutafuta njia za kuzindua upya mchakato wa amani wa DRC, kwa pamoja kwa kuwashirikisha kiongozi wa Congo na mpinzani wake Rwanda, ulifunguliwa Ijumaa pembeni ya mikutano mikuu ya AU na ulipaswa muendelea mpaka Jumamosi.

Forum

XS
SM
MD
LG