Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:22

Nchi zinazozungumza Kifaransa kujadili tatizo sugu la utapiamlo


Watoto wakimbizi kutoka Afrika Kati wakiwa katika kambi ya wakimbizi ya d'Adamaoua, Cameroon. Picha na AFP
Watoto wakimbizi kutoka Afrika Kati wakiwa katika kambi ya wakimbizi ya d'Adamaoua, Cameroon. Picha na AFP

Wafanyakazi wa afya, maafisa na watoa misaada ya kibinaadamu kutoka katika nchi 15 zinazozungumza lugha ya Kifaransa Kusini mwa jangwa la Sahara wanakutana Douala, mji mkuu wa kiuchumi wa Cameroon kujadili tatizo sugu la utapiamlo katika eneo hilo.

Wengi wa watoto katika maeneo yenye mzozo wamekoseshwa makazi kuanzia Sudan na nchi nyingine zilizogubikwa na migogoro. Utapiamlo wao sugu, walisema katika mkutano, umechangiwa na majanga ya hali ya hewa ambayo yanafanya chakula na maji salama kuzidi kuwa haba Kusini mwa Jangwa la Sahara.

“Mashirika yote ya Umoja wa Mataifa yana wasiwasi kuwa mamilioni kadhaa ya watoto wenye utapiamlo wa hali ya juu Kusini mwa Jangwa la Sahara wako hatarini kufariki kabla ya kusheherekea miaka mitano ya kuzaliwa.” alisema Simeon Nanama, mshauri wa lishe wa UNICEF kwa kanda za Kusini na Kati za Afrika.

“Takriban watoto milioni 7 walioathiriwa na utapiamlo wanahitaji sana msaada ili kuokoa maisha yao.”

Mwezi Desemba, maafisa wa Cameroon waliongelea idadi kubwa ya uhamiaji wa wanawake na watoto wanaokimbia ghasia za kijamii na magaidi wa Boko Haram walioko Cameroon, Chad na Nigeria pamoja na nchi nyingine.

Wiki iliyopita, rais wa Chad Mahamat Idris Deby, alitangaza dharura ya chakula na lishe katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati. Deby aliomba msaada wa kimataifa, hususani kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano, ambao amesema wamezidiwa na utapiamlo.

Umoja wa Mataifa umesema utapiamlo ni sababu ya pili inayoongoza kwa vifo miongoni mwa watoto baada ya malaria katika mataifa ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Forum

XS
SM
MD
LG