Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 20:07

Watu wafariki kwa njaa Sudan –WFP


Baadhi ya watu wakisubiri kupokea misaada kutoka shirika la kujitolea la Gedaref, Decemba 30, 2023. Picha na AFP.
Baadhi ya watu wakisubiri kupokea misaada kutoka shirika la kujitolea la Gedaref, Decemba 30, 2023. Picha na AFP.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema Ijumaa, limekuwa likipokea taarifa ya vifo vya watu vinavyotokana na njaa nchini Sudan, na idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa imeongezeka mara dufu kuanzia mwaka jana, wakati vita vikiwa ni kizuizi cha watu kupokea misaada

WFP imeyataka makundi yanapigana, jeshi la Sudan na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) kutoa uhakikisho wa haraka bila kizuizi kwa usambazaji wa misaada.

Takriban watu milioni 18 nchini Sudan wanakabiliwa na njaa kali, na zaidi ya watu milioni tano katika maeneo yaliathiriwa zaidi na vita wakabailiwa na viwango vya njaa vinavyohitaji msaada wa haraka.

WFP imesema katika taarifa kuwa shirika hilo limeweza kupeleka misaada kwa mtu mmoja kati ya kumi katika maeneo hayo, ambayo yanajumuisha mji mkuu wa Khartoum, mkoa wa Magharibi wa Darfur, na jimbo la El Gezira ambako hivi karibuni limedhibitiwa na RSF.

“Inakuwa vigumu kwa mashirika ya misaada kwenda kutokana na vitisho vya usalama, uimarishaji wa vikwazo vya barabarani, na ushuru na kodi zinazotakiwa,” ilisema taarifa ya WFP.

Vita nchini Sudani vilianza mwezi April 2023 wakati jeshi na RSF mapambano ya kugombania madaraka yalipozuka juu ta mpango wa kuhamisha kuelekea utawala wa kiraia.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG