Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:11

ICC yafahamishwa kuwa Sudan na RSF huenda wanatekeleza uhalifu wa kibinadamu


Watu wakitoroka mapigani Magharibi mwa Darfur
Watu wakitoroka mapigani Magharibi mwa Darfur

Kiongozi wa mashitaka kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ICC, Jumatatu ameambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba “uchunguzi wake’ umeweka misingi ya kuamini kwamba jeshi la Sudan, na hasimu wake RSF, wanatekeleza uhalifu wa kibinadamu.

Hayo yamedaiwa kutekelezwa magharibi mwa Darfur, wakati mapigano yakiendelea nchini humo. Karim Khan ambaye hivi karibuni alizuru nchi jirani ya Chad, ambako maelfu ya wakazi wa Darfur wametorokea, alionya kwamba wengi wa wakimbizi aliokutana nao wanahofia Darfur itakuja kusahaulika kutokana na maafa yanayoendelea.

Aliomba serikali ya Sudan kutoa vibali visivyo na masharti kwa wachunguzi wake kuingia nchini, pamoja na kushugulikia maombi 35 ya usaidizi yaliotolewa. Sudan ilitumbukia kwenye ghasia Aprili mwaka jana baada za taharuki ya muda mrefu kati ya jeshi la serikali likiongozwa na Jenerali Abdel Fattah Burhan na kundi la kijeshi la Rapid Support Forces, chini ya Mohammed Hamdan Dagalo kugeuka na kuwa vita kwenye mitaa ya Khartoum, pamoja na maeneo mengine.

Darfur ambayo imekumbwa na mauaji tangu 2003 imekuwa kitovu cha ghasia za sasa ambapo vikosi vya RSF na wapiganaji wa kiarabu wamekuwa wakishambulia makabila ya kiafrika.

Forum

XS
SM
MD
LG