Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:30

Umoja wa Mataifa: Zaidi ya watu 14,000 waliuwawa katika mkoa wa  Darfur nchini Sudan

Wodi iliyojaa majeruhi katika hospitali ya El Fasher katika eneo la Darfur Kaskazini tarehe 21, 2023. Picha na Ali SHUKUR / Médecins sans Frontières (MSF) / AFP.
Wodi iliyojaa majeruhi katika hospitali ya El Fasher katika eneo la Darfur Kaskazini tarehe 21, 2023. Picha na Ali SHUKUR / Médecins sans Frontières (MSF) / AFP.

Kati ya watu 10,000 na 15,000 waliuawa katika mji mmoja kwenye mkoa wa  Darfur Magharibi nchini Sudan mwaka jana katika ghasia za kikabila na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) na wanamgambo washirika wa Kiarabu, kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo  Reuters imeiona siku ya Ijumaa.

Katika ripoti hiyo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wafuatiliaji huru wa vikwazo wa Umoja wa Mataifa walisema idadi hiyo ya El Geneina ilitokana na vyanzo vya kijasusi na kuitofautisha na makadirio ya Umoja wa Mataifa kwamba takriban watu 12,000 wameuwawa kote Sudan tangu vita vilipozuka Aprili 15, 2023 kati ya Jeshi la Sudan ja kikosi cha RSF.

Wachunguzi pia walieleza kama shutuma za kuaminika kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu ulikuwa umetoa msaada wa kijeshi kwa RSF mara kadhaa kwa wiki kupitia Amdjarass kaskazini mwa Chad. Jenerali mkuu wa Sudan aliishutumu UAE mwezi Novemba kwa kuunga mkono juhudi za vita vya RSF.

Katika barua kwa waangalizi hao, UAE ilisema kuwa ndege 122 zimepeleka misaada ya kibinadamu kwa Amdjarass kuwasaidia Wasudan wanaokimbia vita. Umoja wa Mataifa unasema takriban watu 500,000 wameikimbia Sudan na kuelekea mashariki mwa Chad, mamia ya kilomita kusini mwa Amdjarass.

Forum

XS
SM
MD
LG