Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:27

Watu wenye bunduki washambulia vijiji kwenye eneo linalozozaniwa na Sudan na Sudan Kusini


Watu waliokoseshwa makazi kufuatia mashambulizi kwenye vijiji vya Sudan.Picha ya maktaba.
Watu waliokoseshwa makazi kufuatia mashambulizi kwenye vijiji vya Sudan.Picha ya maktaba.

Watu wenye bunduki walishambulia wanavijiji kwenye eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Abyei, linalozozaniwa kati ya Sudan na Sudan Kusini, na kuuwa takriban watu 52, akiwemo mlinda amani wa Umoja wa Mataifa na kujeruhi wengine 64.

“Madhumuni ya shambulizi hilo la Jumamosi usiku hayajabainishwa, lakini inashukiwa ni kutokana na mzozo wa ardhi,” Bulis Koch, ambaye ni waziri wa habari wa jimbo la Abiye, ameambia shirika la habari la AP kwa njia ya simu.

Ghasia zilizopelekea mauaji zimekuwa zikitokea mara kwa mara kwenye eneo hilo, ambako watu wa kabila la Twic Dinka kutoka jimbo jirani la Warrap wamekuwa kwenye mvutano wa ardhi na kabila la Ngok Dinka la Abyei, kutokana na eneo la Aneet karibu na mpaka.

Waliofanya mashambulizi ya Jumamosi walikuwa vijana kutoka kabila la Nuer ambao walihama kutoka jimbo la Warrap mwaka jana kufuatia mafuriko, ameongeza waziri Koch. Kupitia taarifa, kikosi cha muda cha UN, cha kulinda usalama katika eneo la Abiye, UNISFA, kimekemea shambulizi hilo ambalo limesababisha kifo cha mfanyakazi wake.

Forum

XS
SM
MD
LG