Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 15:17

UN yaomba dola bilioni 4.1 kukidhi mahitaji ya kibinadamu Sudan


Kambi ya wakimbizi ya Ourang Decemba 7, 2023. Picha na Denis Sassou Gueipeur / AFP
Kambi ya wakimbizi ya Ourang Decemba 7, 2023. Picha na Denis Sassou Gueipeur / AFP

Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano umezitaka nchi kutowasahau raia waliojikuta katikati ya vita nchini Sudan, ikiomba dola bilioni 4.1 kukidhi mahitaji yao ya kibinadamu na kuwasaidia wale waliokimbilia nchi jirani.

Miezi kumi ya vita huko Sudan kati ya vikosi vya jeshi na vya wanamgambo wa Msaada wa Dharura vimeharibu miundo mbinu ya nchi hiyo na kusababisha maonyo ya njaa na ukosefu wa makazi kwa mamilioni ya watu ndani na nje ya nchi.

Nusu ya idadi ya watu wa Sudan- takriban watu milioni 25- wanahitaji misaada ya kibinadamu na ulinzi, wakati zaidi ya watu milioni 1.5 wamekimbilia Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chadi, Misri, Ethiopia na Sudan Kusini, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Katika kuzindua ombi lake la pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Uratibu wa Mya Kibinadamu (OCHA), imeomba ufadhili wa dola bilioni 2.7 kwa ajili ya misaada kwa watu milioni 14.7.

“Sudan inazidi kusahauliwa na jumuiya ya kimataifa” mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths aliwaambia wanadiplomasia katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi limeomba dola bilioni 1.4 kuwasaidia watu takriban milioni 2.7 katika nchi tano zilizoko jirani na Sudan ikiwa ni sehemu ya ombi hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG