Msururu wa ufyatuaji wa risasi uliua mtu mmoja na kujeruhi wengine 21 Jumatano nje ya kituo kikuu cha reli katika mji wa Kansas, jimbo la Missouri, hapa Marekani, ambapo mabingwa wa mwaka huu wa mashindano ya mpira wa miguu Marekani (NFL), Chiefs, walikuwa wakisherekea ushindi wao wa Super Bowl.