Taifa hilo la Afrika Magharibi lilitumbukia katika mzozo wa kisiasa ambao haujawahi kutokea baada ya Sall kuahirisha uchaguzi ambao awali ulipangwa kufanyika Februari 25.
Pendekezo la tarehe mpya ya uchaguzi linafuatia siku mbili za mazungumzo yaliyoandaliwa na Sall ili kupunguza mvutano.
Mpango wake na ule wa bunge wa kuahirisha uchaguzi wa Februari 25 kwa kipindi cha miezi 10 ulichochea machafuko.
Pendekezo hilo litawasilishwa kwa Sall ambaye atafanya maamuzi ya mwisho, Paye aliiambia Reuters.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika mjini Dakar yalisusiwa na wapinzani wengi, baadhi yao wakitaka uchaguzi ufanyike kabla ya muhula wa Sall kumalizika hapo tarehe 2 Aprili.
Forum