Nchi hiyo ya Afrika Magharibi imekuwa chini ya utawala wa kijeshi tangu maafisa kunyakua mamlaka katika mapinduzi ya Septemba 2021.
Jumuiya kuu ya kiuchumi na kisiasa katika kanda hiyo, ECOWAS, imekuwa ikishinikiza utawala huo, mojawapo ya tawala kadhaa za kijeshi katika ukanda huo, kufanya uchaguzi ndani ya muda unaokubalika na kurejesha utawala wa kiraia.
Pande zote mbili zilikubaliana kuhusu kalenda ya matukio ya mpito ya miezi 24 mnamo Oktoba 2022.
Katibu Mkuu wa afisi ya rais, Amara Camara, bila kutarajiwa alitangaza Jumatatu kwamba serikali ilikuwa imevunjwa.
Bila kueleza sababu za hatua hiyo, alisema katika video iliyorekodiwa awali kwenye mitandao ya kijamii ya ofisi ya rais, kuwa wakurugenzi wa baraza la mawaziri, katibu mkuu na manaibu wao ndio watakaohikilia uongozi hadi serikali mpya itakapoundwa.
Forum