Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 16:53

Rais wa Senegal akubali kuandaa tarehe mpya ya Uchaguzi


Waandamanaji wakikimbia mabomu ya kutoa machozi huko Dakar February 16, 2024. Picha na JOHN WESSELS / AFP
Waandamanaji wakikimbia mabomu ya kutoa machozi huko Dakar February 16, 2024. Picha na JOHN WESSELS / AFP

Rais wa Senegal Macky Sall amesema siku ya Ijuumaa kuwa atatii kikamilifu uamuzi wa mahakama uliyobatilisha kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais hadi Desemba, akiahidi kufanya mashauriano kuandaa uchaguzi haraka iwezekanavyo.

Mswada ambao ulibadilisha tarehe ya uchaguzi wa Februari 25 na kutumbukiza nchi katika mvutano mkubwa wa kisiasa, ulibadilishwa siku ya Alhamisi na Baraza la Katiba la Senegal.

Sall "amezingatia" uamuzi wa baraza wa kutaka uchaguzi ufanyike kwa haraka iwezekanavyo. “Rais anania ya kutekeleza kikamilifu uamuzi huo,” ofisi ya rais imesema siku ya Ijumaa.

Sall yuko katika shinikizo kubwa la kuheshimu uwamuzi huo. Mzozo wa uchaguzi wa wiki mzima umeshababisha maandamano yenye ghasia na tahadhari ya unyanyasaji wa kimabavu katika moja wapo ya mataifa yenye utulivu katika kanda iliyokumbwa na mapinduzi.

Viongozi wa upinzani, jumuiya kuu ya kiunchimi na kisiasa ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS, na mataifa ya kigeni ikijumuisha Marekani na Ufaransa zimewaihimiza maafisa wa serikali mapema Ijumaa kutii uamuzi huo na kutangaza haraka tarehe mpya ya uchaguzi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG