Taifa dogo la visiwa vya bahari ya Hindi la Comoro lilikuwa la kwanza kufanya uchaguzi wa rais mwaka 2024. Rais aliyeko madarakani Azali Assoumani - afisa wa zamani wa jeshi aliyekuchukua madaraka kwa mara ya kwanza mwaka 1999- alishinda awamu yake ya nne kwenye uchaguzi huo ulokua na utata.
Matokeo ya uchaguzi mara moja yalikataliwa na wapinzani, na kuibua maadamano yenye ghasia yaliyosababisha kifo cha mtu mmoja na watu 25 kujeruhiwa.
Nchi inayofuata katika orodha ilitakiwa kuwa Mali, ikifuatiwa na Senegal, lakini uchaguzi katika nchi hizo uliahirishwa. Mali iko chini ya utawala wa kijeshi unaongozwa na Kanali Assimi Goita, tangu 2020.
Wakati huo, Goita aliahidi kurejesha nchi katika utawala wa kiraia lakini hatimaye alifanya mapinduzi kwa mara ya pili miezi kadhaa baadaye, na kumlazimisha kuondolewa madarakani viongozi wa utawala wa mpito walochaguliwa na raia.
Edgar Githua wa chuo kikuu cha kimataifa cha Marekani- Afrika aliiambia Sauti ya Amerika kuwa uchaguzi hautafanyika katika nchi za Sahel ambazo zimekumbwa na mapinduzi.
“Burkina Faso, Mali, Niger, ziliahidi kuingia katika kipindi cha mpito, hawatafanya…Hawa wanajeshi wote wamepewa mafunzo ya kijeshi, hawajui kutawala. Njia ya kujifunza jinsi ya kutawala ni ndefu sana”
Na mapema mwezi huu, katika hatua ambayo haikutarajiwa, rais wa Senegal Macky Sall alitangaza kuwa uchaguzi utacheleweshwa kwa sababu ya madai ya rushwa kutokana na kesi zinazohusiana na uchaguzi na kuenguliwa kwa baadhi wagombea wanaoongoza
Forum