Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 13:12

Mali yasema haitasubiri mwaka uishe kujiondoa ECOWAS


Kiongozi wa kijeshi nchini Mali Assimi Goita alipowasili Saint Petersburg Julai 26, 2023.Picha na AFP
Kiongozi wa kijeshi nchini Mali Assimi Goita alipowasili Saint Petersburg Julai 26, 2023.Picha na AFP

Mali imesema haitosubiri mwaka kuondoka katika Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kama inavyotakiwa kulingana na mkataba wa jumuiya hiyo.

Mali na majirani zake Niger na Burkina Faso, zote zikiongozwa na utawala wa kijeshi, zilitangaza mwezi uliopita kuwa zinajiondoa haraka kutoka ECOWAS, kambi kuu ya kisiasa na kiuchumi kwa nchi za Afrika Magharibi.

Awali nchi zote ziliiarifu tume ya ECOWAS kuhusiana na uamuzi wao wa kujiondoa katika umoja huo katika taarifa ya maandishi ya Januati 29, ambayo kulingana na mkataba inamaanisha wanatakiwa wabaki kuwa wanachama mpaka baada ya mwaka mmoja kuanzia tarehe ya taarifa ya maandishi ilipotolewa.

Katika taarifa iliyobandikwa kwenye mtandao, wizara ya mambo ya nje ya Mali imesema kuwa ECOWAS imekiuka waraka wake wenyewe kwa kufunga mipaka yake kwa Mali wakati ilipoweka vikwazo dhidi ya utawala wa kijeshi. “Matokeo yake, Serikali ya Jamhuri ya Mali haikubaliani na vikwazo vya tarehe ya mwisho vilivyotajwa katika kifungu cha 91 cha mkataba uliofanyiwa marekebisho.” Taarifa hiyo ilisema.

Hakuna majibu ya haraka kutoka ECOWAS au kutoka Niger na Burkina Faso endapo kama watafanya hivyo pia. ECOWAS imepanga kufanya kukutana Febuari 8, kujadili hali hiyo.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG