Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 08:47

Kiongozi wa Chad yuko Russia kutokana na mwaliko wa Putin


Rais wa baraza ya mpito Chad, Mahamat Idriss Deby Itno alipowasili katika sherehe za miaka 63 ya uhuru wa nchi hiyo Agosti 11,2023. Picha na Denis Sassou Gueipeur / AFP
Rais wa baraza ya mpito Chad, Mahamat Idriss Deby Itno alipowasili katika sherehe za miaka 63 ya uhuru wa nchi hiyo Agosti 11,2023. Picha na Denis Sassou Gueipeur / AFP

Rais wa serikali ya mpito wa Chad Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno ameanza ziara Jumanne nchini Russia “kutokana na mwaliko” wa rais wa Russia Vladimir Putin, nchi hizi mbili zimetangaza.

Deby "ameondoka N’Djamena asubuhi Jumanne kwenda Moscow kutokana na mwaliko wa rais Vladimir Putin. Mkuu wa nchi amechukua jukumu la kufanya safari hiyo rasmi ya kuutembelea mji mkuu wa Russia.”

Kremlin imethibitisha ziara hiyo na mkutano wa Jumatano kati ya viongozi hao wawili, ikismesema watajadili “mitazamo ya maendeleo ya uhusiano kati ya mataifa ya Russia na Chad katika nyanda mbalimbali, ikiwemo masuala ya hivi sasa ya kikanda na kimataifa.”

Chad ambayo jeshi la Ufaransa bado lina wanajeshi wake huko, ni mshirika pekee aliyebaki katika kanda hiyo ya Sahel baada ya kulazimishwa kuyaondoka majeshi yake nchini Mali mwezi Agosti 2022, Burkina Faso mwezi Februari 2023 and Niger mwezi Decemba.

Those three countries have since all moved closer to Russia, especially militarily following the end of Operation Barkhane which ran from 2014 to 2022 and saw France lead a military counterinsurgency against Islamic insurgents in the Sahel.

Nchi hizo tatu tangu wakati huo zimekuwa zikijisogeza kuwa karibu na Russia, hususani kijeshi baada ya kumalizika kwa operesheni Barkhane ambayo ilianza mwaka 2014 mpaka mwaka 2022 na kuona Ufaransa ikiongoza jeshi katika mapambano dhidi ya makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali katika kanda hiyo ya Sahel.

Forum

XS
SM
MD
LG