Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 05:15

Nigeria yakosoa hatua ya Mali, Niger na Burkina Faso, ya kujiondoa kwenye ECOWAS


Mawaziri wa Ulinzi kutoka mataifa wanachama wa ECOWAS isipokuwa wale kutoka Mali, Burkina Faso, Chad, Guinea na Niger wakiwa kwenye mkutano wa Ghana, Januari 28, 2024.
Mawaziri wa Ulinzi kutoka mataifa wanachama wa ECOWAS isipokuwa wale kutoka Mali, Burkina Faso, Chad, Guinea na Niger wakiwa kwenye mkutano wa Ghana, Januari 28, 2024.

Nigeria Jumatatu imesema kwamba viongozi wa kijeshi wasiochaguliwa na raia wa Niger, Mali na Burkina Faso wamewasaliti watu wao, kufuatia uamuzi wa pamoja wa kujiondoa kwenye shirika la kiuchumi la mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Nigeria ambayo ni mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS, imezungumza kwa mara ya kwanza baada ya mataifa hayo kutangaza Jumapili kwamba yamejiondoa kwenye shirika hilo, ambalo limekuwepo kwa karibu miaka 50.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Nigeria kupitia taarifa imesema kwamba wale wanaokusudia kujiondoa kwenye ECOWAS, hawafanyi hivyo kwa nia njema. “Badala yake viongozi ambao hawajachaguliwa wameamua kuhujumu haki ya wananchi ya uhuru wa kutembea, wa kufanya biashara, pamoja na uhuru wa kuchagua viongozi wao.

Kufia sasa ECOWAS haijatoa taarifa yoyote kufutia tangazo la kujiondoa kwa mataifa hayo. Hata hivyo Nigeria imeongeza kwamba ipo tayari kushauriana na mataifa yote matatu kuhusu suala hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG