Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:25

Rais Geingob wa Namibia azikwa Jumapili


Maelfu ya wakazi wa Namibia waliohudhuria mazishi ya Rais Hage Geingob, kwenye bustani ya Heroes Acre mjini Windhoek.
Maelfu ya wakazi wa Namibia waliohudhuria mazishi ya Rais Hage Geingob, kwenye bustani ya Heroes Acre mjini Windhoek.

Aliyekuwa rais wa Namibia Hage Geingob ambaye alifariki akiwa hospitalini  Februari 4, wiki kadhaa baada ya kupatikana na saratani, amezikwa kwenye bustani ya mashujaa ya Heroes Acre, Jumapili, huku maelfu ya watu wakihudhuria wakiwemo viongozi 25 wa mataifa, pamoja na marais wa zamani.

Mazishi hayo yamefanyika viungani mwa mji mkuu wa Windhoek, baada ya siku 20 za maombolezo, huku wanajeshi wakifyatua mizinga 21 kwa heshima yake, wakati ndege za kivita za kijeshi zikipaa angani kwenye eneo hilo.

Geingop aliyekuwa na umri wa miaka 82 aliwahi kuwa waziri mkuu wa taifa hilo mara mbili, na baadaye kuwa rais wa 3 wa taifa hilo tangu kujipatia uhuru wake kutoka Afrika Kusini 1990. Utawala wake wa taifa hilo lenye watu wachache na ambalo sehemu kubwa ni jangwa, ulianza 2015.

Akiwa mmoja wa wanaharakati wa uhuru, Geingop alikimbilia kwenye mataifa ya kigeni kwa miaka 27, yakiwemo Botswana, Zambia na Marekani, kabla ya kurejea nchini 1989. Iliwahi kuhudumu kwenye nyadhifa mbali mbali serikalini, pamoja na kwenye chama tawala cha South West African People’s Organisation, SWAPO.

Forum

XS
SM
MD
LG