Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:40

Kamandi Kuu ya jeshi la Marekani yakamata silaha zikielekea Yemen


Kamandi Kuu yakamata meli ilibeba silaha za Iran zikisafirishwa katika meli kwenda kwa Wahouthi, Yemen.
Kamandi Kuu yakamata meli ilibeba silaha za Iran zikisafirishwa katika meli kwenda kwa Wahouthi, Yemen.

Majeshi ya Marekani yamekamata silaha za kisasa za kivita na misaada mingine ya silaha za nzito kutoka Iran ambazo zilizokuwa zinaelekea maeneo yanayo shikiliwa na Wahouthi nchini Yemen.

Silaha hizo zilikuwa zinasafirishwa kwa meli katika Bahari ya Arabia Januari 28, Kamandi Kuu ya jeshi la Marekani ilisema katika taarifa yake Alhamisi.

Zaidi ya vifurushi 200 vilivyokuwa na vifaa vya kutengeneza makombora ya masafa ya kati ya balistiki, vilipuzi, malighafi za magari yasiyokuwa na dereva ya chini ya maji na juu ya ardhi (UUV/USV), vifaa vya mawasiliano na mitandao yenye hadhi ya kijeshi, malighafi ya mifumo ya kurushia makombora ya kuharibu vifaru, na vifaa vingine vya kijeshi viligunduliwa katika meli hiyo, ilisema taarifa.

Hatua ya Iran kuendelea kupeleka silaha za kisasa za kivita kwa Wahouthi inaendelea kuhujumu usalama wa meli za kimataifa na usafirishaji wa bidhaa za biashara,” Kamanda wa Kamandi Kuu ya Marekani Michael Erik Kurilla alisema.

Wanamgambo wa Kihouthi nchini Yemen wamekuwa wakishambulia mara kwa mara meli za biashara za kimatiafa kwa kutumia droni na makombora tangu katikati ya Novemba, wakisema wanafanya hivyo kuwaunga mkono Wapalestina dhidi ya hatua za kijeshi za Israeli huko Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG