Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:28

Wahouthis wafyatua makombora kwa meli mbili katika Bahari ya Sham


Picha iliyochapishwa na jeshi la wanamaji la India, inaonyesha meli ya Marekani iliyoshambuliwa na ndege isiyokuwa na rubani ya Wahouthis, Januari 18, 2024.
Picha iliyochapishwa na jeshi la wanamaji la India, inaonyesha meli ya Marekani iliyoshambuliwa na ndege isiyokuwa na rubani ya Wahouthis, Januari 18, 2024.

Waasi wa Yemen Wakihouthi wanaoungwa mkono na Iran Jumanne wamesema walishambulia kwa makombora meli mbili katika Bahari ya Sham, na kusababisha uharibifu mdogo kwa meli moja ya mizigo iliyokuwa ikisafiri kutoka pwani ya Hodeidah nchini Yemen.

Wahouthi wamekuwa wakilenga meli za biashara kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani na makombora katika Bahari ya Sham tangu katikati mwa mwezi Novemba, katika kile walichokielezea kama hatua za mshikamano na Wapalestina dhidi ya Israel katika vita vya Gaza.

Msemaji wa kijeshi wa kundi hilo amesema wamefyatua makombora kwa meli za Morning Tide na Star Nasia, akizitaja meli hizo zilikuwa na bendera ya visiwa vya Barbados na Marshall, ambavyo viko chini ya mamlaka ya Uingereza na Marekani.

Kampuni ya usalama wa baharini ya Uingereza ya Ambrey imesema meli ya mizigo iliyokuwa na bendera ya Barbados inayomilikiwa na kampuni ya Uingereza iliharibiwa kutokana na shambulio la ndege isiyokuwa na rubani, ilipokuwa ikisafiri kusini mashariki kupitia Bahari ya Sham.

Hakuna majeruhi walioripotiwa. Meli hiyo ilitumia mbinu kukwepa na kuendelea na safari yake, kampuni ya Ambrey imesema.

Forum

XS
SM
MD
LG