Afrika Kusini itatuma wanajeshi 2,900, kama sehemu ya mchango wake kwa kikosi cha Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kinachotarajiwa kukabiliana na makundi yenye silaha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ofisi ya rais Cyril Ramaphosa, ilisema katika taarifa yake Jumatatu.