Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:27

Afrika Kusini yaitaka jumuiya ya kimataifa kusitisha ufadhili kwa jeshi la Israeli


Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani Naledi Pandor
Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani Naledi Pandor

Huku vita kati ya wanamgambo wa Hamas na Israeli vikiingia mwezi wa nne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kusitisha ufadhili kwa jeshi la Israeli.

Waziri huyo, Naledi Pandor, amesema Mahakama ya Kimataifa ya Haki imeashiria kuwa mauaji ya kimbari yanafanyika katika ukanda wa Gaza, kama ambavyo serikali ya Rais Cyril Ramaphosa, ilidai kwenye nyaraka ilizowasilisha katika mahakama hiyo.

Pandor amesema kuna umuhimu kwa mataifa mbalimbali duniani kuacha kutoa kufadhili na kuwezesha hatua za kijeshi za Israel katika ukanda wa Gaza, akinukuu uamuzi wa hivi karibuni wa mahakama ya ICJ.

"Uamuzi huo, tunadhani, pia unaweka wazi kuwa ni kweli kwamba mauaji ya kimbari yanafanyika...," alisema Waziri Pandor

Pandor alikuwa akizungumza baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki wiki iliyopita kuamuru Israel kuchukua hatua zote katika uwezo wake kuzuia wanajeshi wake kufanya mauaji ya halaiki.

"Hii lazima inaweka wajibu kwa mataifa yote kusitisha ufadhili na kuwezesha hatua za kijeshi za Israeli, ambazo, kama mahakama ilivyoonyesha, ni mauaji ya halaiki," aliongeza.

ICJ nusra iamuru kusitishwa kwa mapigano, kama ilivyoombwa na Afrika Kusini kama mlalamikaji, lakini pia iliitaka Israel kuchukua hatua za kuboresha hali ya kibinadamu ya Wapalestina huko Gaza.

Kwa mujibuu wa shirika la habari la Reuters, huenda ikachukua miaka kadhaa kabla ya uamuzi kuhusu iwapo Israeli inatekeleza mauji ya kimbari katika ukanda wa Gaza kuamriwa na mahakama hiyo juu ya kiini cha kesi ya Afrika Kusini - kama mauaji ya halaiki yametokea katika ukanda wa Gaza.

Afrika Kusini kwa miongo kadhaa imekuwa mtetezi wa Palestina ambayo inalinganisha hali inayoendelea na mapambano ya watu Weusi wa Afrika Kusini dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Israel imekanusha hilo na imekanusha madai ya mauaji ya halaiki.

Katika uamuzi wake wiki jana, ICJ ilisema ina mamlaka ya kutoa uamuzi juu ya hatua za dharura, na kuongeza kwamba haitatupilia mbali kesi ya mauaji ya halaiki kama Israeli ilivyoomba.

Ilibainisha kuwa Wapalestina wanaonekana kuwa kundi linalolindwa chini ya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari, na kusisitiza kuwa inatambua haki ya Wapalestina huko Gaza kulindwa dhidi ya vitendo vya mauaji ya kimbari.

Miongoni mwa hatua ambazo Afrika Kusini iliomba ni kusitishwa mara moja kwa mashambulizi ya kikatili ya Israel, ambayo yameharibu sehemu kubwa ya eneo hilo na kuua zaidi ya Wapalestina 26,000, kulingana na mamlaka ya afya ya Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG