Sikhala mwenye umri wa miaka 51 na ambaye ni mkosoaji mkubwa wa serikali, ni miongoni mwa viongozi mashuhuri kukamatwa katika miaka ya karibuni, kutokana na kile mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema ni msako dhidi ya wapinzani kwenye taifa hilo la Kusini mwa Afrika.
“Hiki kili kitendo cha kuadibishwa.” Sikhala aliambia vyombo vya habari vya ndani, muda mfupi baada ya kuachiliwa jela iliyopo kwenye vitongoji vya Harare. “Wale walionizuilia kwenye jela hii kwa muda mrefu ni vyema wafahamu kwamba nipo tayari kulipia gharama yoyote ile kutokana na upendo mwingi niliyo nao kwa taifa langu,” amesema Sikhala.
Akiwa wakati mmoja mbunge, Sikhala, pamoja na mbunge wa sasa wa upinzani Godfrey Sithole walihukumiwa wiki iliyopita kutokana na tuhuma za kuchochea umma. Hata hivyo Jumanne wamepewa kifungo cha nje cha miaka miwili kila mmoja. Kundi ndogo la wafuasi wao lilikusanyika nje ya mahakama kusherehekea uamuzi huo.
Forum