Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:19

Afrika Kusini yadai Israel imekaidi amri ya mahakama


Mmoja wa waandamanaji wanaounga Palestina mkono nje ya Mahakama ya ICJ.
Mmoja wa waandamanaji wanaounga Palestina mkono nje ya Mahakama ya ICJ.

Afrika Kusini kupitia waziri wake wa Mambo ya Kigeni Naledi Pandor, imesema Jumatano kwamba Israel imekaidi uamuzi wa wiki iliyopita kutoka mahakama ya Umoja wa Mataifa, kwa kuendelea kuuwa mamia ya raia ndani ya muda wa siku chache huko Gaza.

Taifa hilo pia limehoji ni kwa nini hati ya kukamatwa kwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu haijatolewa, kupitia kesi tofauti iliyowasilishwa mbele ya mahakama ya ICC.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Pandor amesema kwamba Afrika Kusini inatadhmini kupendekeza hatua mbadala kwa jumuia ya kimataifa, ili kushinikiza Israel kusitisha mauaji ya raia kwenye vita vyake vya Gaza dhidi ya wanamgambo wa Hamas, ingawa hakutoa maelezo zaidi.

Tangu uamuzi wa mahakama ya ICJ mwishoni mwa wiki kwamba Israel isitishe mauaji hayo, mamia ya wapalestina wameuwawa kulingana na wizara ya afya ya Gaza. Wizara hiyo imeongeza kwamba watu 150 waliuwawa kwenye eneo hilo ndani ya saa 24, na kufikisha jumla ya wapalestina waliokufa tangu mwanzo wa mapigano hayo kuwa 26,700.

Forum

XS
SM
MD
LG