Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 16:46

Chama tawala nchini Afrika Kusini chamsimamisha rais wa zamani Zuma


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Chama tawala nchini Afrika Kusini Jumatatu kimemisimamisha kwenye chama rais wa zamani Jacob Zuma na kuapa kuwasilisha mashtaka dhidi ya kundi pinzani linalofanya kampeni kwa jina lake.

Akitangaza uamuzi huo, katibu mkuu wa ANC Fikile Mbalula amesema” Zuma na wengine ambao mwenendo wao unakinzana na maadili na kanuni zetu, watajikuta nje ya chama cha African National Congress.”

Zuma alikuwa rais wa nne wa Afrika Kusini yenye utawala wa kidemokrasia kuanzia 2009 hadi 2018, lakini alilazimishwa kujiuzulu chini ya wingu la tuhuma za ufisadi na alijitenga na chama alichokiongoza.

Mwezi Disemba, alitangaza kwamba atafanya kampeni kwa niaba ya chama kipya, uMkhonto We Sizwe (MK) au mkuki wa taifa, jina la tawi la kijeshi la chama cha ANC wakati wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Forum

XS
SM
MD
LG