New York na New Jersey kwa pamoja ziling’ang’ania nafasi hiyo, huku zikikabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Texas, ili kuwa wenyeji wa mchuano utakaofanyika tarehe 19, mwezi, kama kilele cha mashindano yaliyopanuliwa ya timu 48, yakiandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico.
Mashindano hayo yataanza kwa mechi ya ufunguzi kwenye Uwanja wa Azteca mjini Mexico City, nchini Mexico, tarehe 11, mwezi Juni mwaka huo. Atlanta na Dallas watakuwa wenyeji wa nusu fainali huku mechi ya kumtafuta nambari tatu uikifanyika mjini Miami, jimbo la Florida.
Michuano ya robo fainali itafanyika Los Angeles, Kansas City, Miami na Boston. Jumla ya miji 16 katika nchi hizo tatu itakuwa wenyeji wa michuano mbalimbali, huku sehemu kubwa ya mechi hizo, zikichezewa nchini Marekani.
Uamuzi wa Jumapili ulitangazwa moja kwa moja kwa njia ya televisheni katika hafla iliyohudhuriwa na Rais wa FIFA Gianni Infantino pamoja na mcheshi na mwigizaji Kevin Hart, rapper Drake, na msanii mashuhuri wa Marekani Kim Kardashian.
Forum