Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 07:07

Mahakama yaamua Trump hana kinga kwa mashtaka ya njama ya kubadilisha matokeo


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Mahakama ya Rufaa ya Serikali Kuu imetoa uamuzi kuwa Donald Trump hana kinga kwa mashtaka ya kuhusika na njama ya kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa 2020 alioshindwa, ikimsogeza rais wa zamani wa Marekani karibu zaidi na kesi ya uhalifu ambayo haijawahi kutokea.

Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa ya Marekani ya District of Columbia Circuit ilitupilia mbali madai ya Trump kwamba hawezi kushtakiwa kwa sababu madai hayo yanahusiana na majukumu yake rasmi alipokuwa rais.

Uamuzi huo, ambao bila shaka Trump atakata rufaa, unatupilia mbali jaribio lake la kuepuka kesi kwa mashtaka ya kuwa alihujumu demokrasia ya Marekani na makabidhiano ya madaraka, licha ya kuendelea kujizatiti katika nafasi yake kama mgombea wa mbele wa uteuzi wa nafasi ya urais kwa chama cha Republikan.

Mawakili wa Trump wametoa hoja kuwa marais wa zamani wanastahili kupewa kinga ya kisheria ya jumla na hawawezi kufunguliwa mashtaka ya uhalifu kwa hatua rasmi walizochukua ila kwanza wawe wamefunguliwa mashtaka na Baraza la Wawakilishi na kuondolewa katika wadhifa wao na Baraza la Seneti.

Trump alifunguliwa mashtaka mara mbili na Baraza la Wawakilishi, lakini kila wakati Baraza la Seneti lilipiga kura za kutosha kumuondolea mashtaka yanayomkabili.

Forum

XS
SM
MD
LG