Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 10:36

Jimbo la New Hampshire kufanya uchaguzi wa awali Jumanne


Wagombe urais wa chama cha Republican, rais wa zamani wa Marekani Donald Trump (kushoto) na balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa Nikki Haley (kulia)
Wagombe urais wa chama cha Republican, rais wa zamani wa Marekani Donald Trump (kushoto) na balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa Nikki Haley (kulia)

Jimbo dogo la Kaskazini Mashariki mwa Marekani la New Hampshire litafanya uchaguzi wa awali wa rais Jumanne.

Jimbo hilo, linajivunia uhuru na uwezo wa kuharibu mambo, linavutiwa zaidi ya habari za Jumapili kwamba Gavana wa Florida Ron DeSantis amehitimisha kampeni zake, na kuufanya ushindani kuwa wa watu wawili tu katika chama cha Republican.

Siyo kile ambacho unakitarajia kukisikia kabla ya uchaguzi wa awali wa uteuzi wa mgombea urais. Lakini hili jimbo la New Hampshire, ambako Rais Joe Biden hayuko katika kura ya Jumanne, hatua ya viongozi wa kitaifa wa chama cha Democratic, ambao baadhi wanaona ni dharau.

Kathy Sullivan, ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa chama cha Democratic katika Jimbo hilo amesema,

“Watu wamesema tutaliweka hilo pembeni na kwenda kumuunga mkono Joe Biden kwasababu sote tunafahamu Donald Trump atakuwa mgombea na jambo muhimu tunaloweza kufanya ni kuokoa demokrasia kwa kumzuia Donald Trump.”

Rais Joe Biden akisalimiana na watu wakati alipokutana na mameya huko White House Januari 19,2024
Rais Joe Biden akisalimiana na watu wakati alipokutana na mameya huko White House Januari 19,2024

Mwenyekiti wa chama cha Democratic New Hampshire, Ray Buckley naye amesema kesho Jumanne, Biden hatapata kura yake. “Tangu kuchaguliwa kama mwenyekiti, nimemuandikia rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter kila wakati kuonyesha kwamba mimi sielemei upande wowote,” alisema.

Buckley aliwapigia kura wagombea urais wa chama cha Democratic waliokuwa madarakani katika miaka iliyopita. Lakini wakati huu amesema Tunashtushwa na kushangazwa”

Kamati ya Kitaifa ya Democrati iliishusha New Hampshire kutoka katika nafasi yake kihistoria kama jimbo la kwanza kuitisha uchaguzi wa awali na kuipendelea South Carolina, ambayo ina mchanganyiko wa wapiga kura.

Maafisa wa chama katika jimbo hilo waliokasirika walipanga hata hivyo uchaguzi wa awali, na wafuasi wa Biden walianza kampeni zao.

Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe Jill Biden baada ya kuhutubia huko Pennsylvania Januari 5, 2024.
Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe Jill Biden baada ya kuhutubia huko Pennsylvania Januari 5, 2024.

Kwa upande wa Republican, aina tofauti ya mchezo imejitokeza. Katika jiji hilo lenye upepo na baridi kali sana, huu ni mstari ambao umejipanga, saa nne kabla ya tukio la Donald Trump.

Derek Levine, Mpiga Kura huko New Hampshire

“Tunampenda Trump, anatupigania sisi.”

Na mpiga kura mwingine wa jimbi hilo Dee Boisvert, pia alisema “Vita vingapi amevifanya wakati alipokuwa rais? Kila mtu alikuwa na furaha kubwa sana, kila mtu alikuwa akijipatia kipato.”

Rais wa zamani Donald Trump anavutia umati wa watu katika mikutano yake na ukusanyaji maoni unamuoneyesha yuko juu kwa asilimia 50 miongoni mwa wapiga kura wa New Hampshire. Balozi wa zamani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley yuko katika asilimia 35 katika ukusanyaji maoni ulifoanywa na Boston Globe.

Denise Montminy, pia ni mpiga kura huru wa New Hampshire anaeleza “Anatakiwa kunisukuma mimi, kwa niko wazi kwa chochote ambacho anaweza kukisema.”

Kama Denise Montminy, wengi waliokuwa kwenye mstari kumuona Haley ana wapiga kura huru au wa chama cha Democratic ambao wanaweza kukipigia kura chama cha Republican hapa New Hampshire.

Mgombe urais kutoka chama cha Republican
Mgombe urais kutoka chama cha Republican

Mpiga kura huru mwingine wa New Hampshire Isaac Geer, naye alisema “Ningependa kusiki matamshi machache sana kuhus vita kutoka kwake katika misingi ya msimamo wake kuhusu Ukraine na vita vya Israel na Palestina.”

Wachambuzi wanasema Warepublican huko New Hampshire, ambao ni waconservative wenye kufuatilia sana masuala ya fedha wana hamu kubwa ya kupunguza kodi na serikali ndogo, huenda Haley akawa ni fursa yao ya mwisho katika kumzuia Trump kugombea.

Naye Profesa Chris Galdieri wa chuo cha St. Anselm alisema “Kama hawezi kufanya katika ambalo amewekewa mambo sawa, nadhani ni vizuri kuuliza, je, hatua inayofuata ni ipi? Katika jimbo gani ambalo anaweza kupata fursa nyingine ya kumshinda Trump, na idadi ya majimbo ambayo naweza kuyataja ni kidogo sana.”

Jumanne usiku, tutafahamu kama wapiga kura wa New Hampshire watatupa chochote cha kutushangaza.

Forum

XS
SM
MD
LG